Pages

Saturday, January 20, 2018

BINTI MWENYE UVIMBE BEGANI AFARIKI DUNIANa Tumaini Msowoya, Mwananchi.

Maria Amrima (17) mkazi wa Mtwara, aliyeanza kupatiwa matibabu Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) jijini hapa kutokana na uvimbe mkubwa begani, amefariki dunia.


Mkurugenzi wa ORCI, Julius Mwaiselage amethibitisha kifo hicho, kwamba taasisi hiyo inaandaa taarifa kamili.


Binti huyo ambaye alitakiwa kufanyiwa upasuaji Muhimbili mwaka mmoja uliopita wakati huo uvimbe ukiwa bado mdogo, alitoweka baada ya kwenda katika tiba za asili kabla ya kurejea hospitalini hapo Januari 3 mwaka huu, baadaye kuhamishiwa katika taasisi hiyo.


Awali jopo la madaktari bingwa kutoka vitengo vitatu vya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Ocean Road, waliungana kwa pamoja kuangalia uwezekano wa kumtibu na kuokoa maisha yake baada ya tiba ya upasuaji kushindikana.
Chanzo - MWANANCHISource

Video Mpya ya Asili : KADO KAMAGU - BHUGAWANinayo hapa ngoma mpya ya Kado Kamagu inaitwa Bhugawa.Video hii imetengenezwa katika studio za Kalunde Media Itazame video hii hapa chiniSource

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Ameondoa Nchini Leo Kuanza Ziara ya Wiki Moja Nchi za Falme za Kiarabu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi,kabla ya kuaza ziara yake katika Nchi za Falme za Kiarabu wakiwa katika chumba cha VIP Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na UsaIama Zanzibar wakati wa kuondoa Zanzibar kuaza ziara yake ya Kiserikali katika Nchi za Falme za Nchi za Kiarabu.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Wazee wa CCM Zanzibar katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kuaza ziara yake ya Wiki moja katika Nchi za Falma za Kiarab.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanziba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar kuaza ziara yake ya Kiserikali katika Nchi za Falme za Kiarabu.

Picha na Ikulu

Source

WABUNGE TANZANIA WATAKIWA KUWASILISHA TAARIFA ZAO ZA MIAMALA YA BENKI

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imewaandikia barua baadhi ya wabunge, ikiwataka kuwasilisha taarifa za miamala ya benki za kuanzia Januari hadi Desemba 2017.


Sekretarieti hiyo imetaka taarifa hizo ziwe zimeifikia ndani ya siku 30 kuanzia Januari 15, 2018.


Barua hiyo inawataka wabunge hao kutekeleza agizo hilo ili kuthibitisha taarifa zilizomo kwenye tamko lake alilowasilisha.


Ofisa mmoja wa taasisi hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, alithibitisha kuwepo kwa barua hizo, akisema si wote walioandikiwa barua za kutakiwa kutoa taarifa hizo.


Hata hivyo, alisema wabunge walioandikiwa ni wale ambao fomu zao zinaonyesha haja ya uhakiki zaidi wa taarifa zao.


Rais wa John Pombe Magufuli ndiye alikuwa wa kwanza kuwasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam Desemba 28, 2017.


Baada ya kuwasilisha fomu hiyo, Rais aliipongeza sekretarieti hiyo kwa kazi inazofanya na kumtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu, Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye angeshindwa kuwasilisha tamko la kabla ya Desemba31, 2017.


Kauli hiyo ya Rais iliwaamsha viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge na viongozi wengine wa Serikali kufurika kwenye ofisi hiyo kuwasilisha matamko yao ya mali walizonazo.

Source

Wafanyakazi wa Nyumbani wataka Elimu ya Afya ya Uzazi kusambazwa zaidi

 Watoto wafanyakazi wa nyumbani Jijini Mwanza wameeleza kwamba suala la ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi ni chanzo kikuu cha tatizo la mimba za utotoni na hivyo kuomba elimu hiyo izidi kutolewa katika makundi mbalimbali ya watoto ili kupambana na tatizo hilo.
Watoto hao waliyasema hayo jana kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wafanyakazi wa nyumbani Jijini Mwanza, kuhusu Elimu ya Afya ya uzazi yaliyoandaliwa na Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyakazi wa Nyumbani nchini WOTESAWA.
"Ukosefu wa elimu ya uzazi, umaskini, tamaa pamoja na makundi maovu yenye ushawishi ni miongoni mwa sababu zinazosababisha mimba za utotoni hivyo mafunzo haya yatatusaidia kuepukana na tatizo hilo". Alisema Christina William ambaye ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo.
Akiwasilisha mada kuhusu mimba za utotoni, Veronica Rodrick ambaye ni Afisa Miradi shirika la WOTESAWA, alisema ni wakati mwafanya wazazi na walezi nchini kuvunja ukimya na kuzungumza na watoto wao kuhusu afya ya uzazi ili kuwanusuru na mimba za utotoni pamoja na magonjwa ya zinaa.
"Tumeamua kuvunja ukimya kwa sababu inaonekana hata huko nyumbani wazazi wanaogoka kukaa na watoto wao kuzungumza juu ya masuala ya afya ya uzazi ikiwemo mimba, virusi vya ukimwi na kinga". Alisisitiza huku akiwahimiza kujiepusha na mapenzi katika umri mdogo, na hata ikitokea mtu ameshindwa kujizuia basi wazingatie matumizi ya kondom.

Katika mada hiyo, kulikuwa na mjadala mpana juu ya matumizi sahihi ya kondom ambapo walihoji ikiwa ni kweli kondomu inazuia mimba pekee ama inazuia pia na magonjwa ya kuambukiza ikiwemo virusi vya ukimwi, hatua iliyoashiria kwamba watoto wengi katika ya miaka 14 hadi 18 bado hawana elimu ya kutosha kuhusu elimu hiyo. Baadhi ya watoto walikuwa wakiamini kwamba kondom inazuia mimba pekee na haiwezi kuzuia virusi vya ukimwi huku wengine wakiamini kondom zina vitundu vidogo vidogo vinavyoweza kupitisha virusi vya magonjwa ya kuambukiza, jambo ambalo si sahihi kwani matumizi sahihi ya kondom huzuia mimba na maambukizo ya magonjwa ya kujamiana.
Source

SERIKALI YATOA TAHADHARI UGONJWA WA HOMA YA 'CHIKUNGUNYA'

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeutahadharisha umma kuhusu ugonjwa wa Homa ya Chikungunya ambao huambukizwa na mbu aina ya aedes na hauna tiba mahsusi wala kinga. Isome taarifa hii kuelewa zaidi kuhusu ugonjwa huo.Source

NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI ZINAVYOIHANGAISHA WILAYA YA MISSENYI

 Mkuu wa Wilaya  Missenyi Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera Luteni kanali Denis Mwila akihutubia katika uzinduzi wa kampeni
 Missenyi,
Jumla ya kesi 31 zimepokelewa na jeshi la polisi wilayani missenyi mkoani kagera  zikihusisha makosa ya mimba pamoja na ndoa za utotoni kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa mwaka 2017
Hayo yamebainishwa na koplo RASHID RAMADHAN afisa wa polisi dawati la jinsia wilayani missenyi alipokuwa akitoa taarifa ya jeshi la polisi wilayani hapa katika uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ndoa za utotoni inayoendeshwa na shirika la World Vision Tanzania
Amesema kuwa kati ya kesi hizo,20 zimeshakamilishwa ushahidhi ka kufikishwa mahakamani,7 watuhumiwa bado wanaendelea kutafutwa na 4 ziko chini ya upelelezi wa jeshi hilo.
Naye afisa ustawi wa jamii wilayani missenyi ANORD NKONGOKI amesema kuwa kwa mwaka 2017 walipokea jumla ya malalamiko 31 yakihusisha  wanafunzi kupatiwa ujauzito ambapo baada ya kuzipokea walilazimika kulishirikisha jeshi la polisi ili kuwatafuta wahalifu na baadhi ya kesi hizo zimekwishafikishwa mahakamani.
Bwana NKONGOKI ameongeza kwa kuzitaja baadhi ya sababu zinazopelekea ndoa pamoja na mimba za utotoni kuwa ni umaskini 
wa kipato kwa wazazi ambapo hulazimika kuwaoza watoto ili wapate mali,tama kwa watoto wa kiike pale wanaporubuniwa na vijana hasa kundi la boda boda sanjari na wazazi kutengana na kupelekea kutowajali watoto
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya missenyi kanali DENICE MWILA amesema kuwa maendeleo ya nchi yamekuwa yakirudishwa nyuma kutokana na wimbi wa mimba za utotoni ambapo watoto hujikuta wakipoteza malengo yao na kusema kuwa serikali wilayani hapa inaendelea na mpango wa kudhibiti janga hilo kwa kuendelea 
na msako kwa vijana wanaojihusisha na vitendo vya kimahusiano pamoja na wanafunzi

Aidha mratibu wa shirika la World Vision Tanzania mkoani Kagera ambalo ndilo linaratibu kampenin hiyo, bwana RENATUS RUGAKINGILA amesema kuwa shirika hilo limeamua kuanzisha kampeni hiyo kufuatia watoto wengi hasa wa kike kupoteza ndoto zao kutokana na janga la ndoa za utotoni na kuongeza kuwa watatoa elimu kwa jamii kila sehemu hasa katika mikutano ya vijiji na mashuleni ili jamii ipate uelewa wa kutosha juu ya athati zinazotokana na ndoa za utotoni.
NA AVITUS MUTAYOBA

Source